MAWAZO CHALLENGE STUDENTS HEALTH INNOVATION

*14/06/2017* Serikali ya wanafunzi kupitia wizara ya afya KIU tunapenda kuwatangazia umma wote wa Kampala kuwa kwa yeyote yule mwenye wazo au idea yeyote inayohusu kada ya afya kwa ujumla anaruhusiwa kujiandikisha na kuapply katika shindano la mawazo challenge linalojumuisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kutoka TANZANIA idea au project hiyo inatakiwa kuwa katika maandishi na kuapply direct katika website husika www.mawazochallenge.com
Kumbuka kuwa shindano hili linahusu wanafunzi wote kutoka kada mbalimbali za afya Tanzania na project au idea itakayoibuka. mshindi itazawadiwa kiasi kisichopungua  2500 pounds sawa na 7.14 millions za kitanzania lakini pia mfuko huu uko tayari kugharamia na kuendeleza project hiyo hadi kufanikiwa.
Wizara ya afya KIU inapenda kutoa fursa kwa wanafunzi wote kukiwakilisha vyema chuo chetu katika mashindano haya, andaa project yako tuma katika website na hakikisha unajisajili katika ofsi za serikali ya wanafunzi kwa waziri husika na mwisho wa kujiandikisha ni siku ya ijumaa tunawakaribisha wote kukiwakilisha chuo chetu.
Sambamba na hilo wizara pia inaendelea kuwakaribisha wanafunzi wote ambao wanauhitaji wa kurenew kadi za bima kuendelea kujisajili ili kuhakikisha zoezi linafanikiwa mapema kwa kunufaisha watu wengi kadri tuwezavyo.
Mwisho wizara hii inapenda kutoa pongezi kwa wanakiu wote kwa namna mnavoshirikiana nasi na kutoa tarifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu afya kupitia changamoto hizo ndipo tunapata utatuzi na tunazidi kuwatakia ndugu zetu wote waislamu mfungo mwemaaa.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na;
*Dickson J Elisha (0785755909)*
*WAZIRI WA AFYA KIUDSO*
Imetolewa na:
*Mhagama David L*
*WAZIRI WA HABARI NA MAWASILIANO*

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *